Wednesday, November 2, 2016

FA YAMFUNGIA MECHI MOJA MENEJA JOSE MOURINHO NA KUTOZWA FAINI YA PAUNDI £50,000


MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amefungiwa Mechi 1 na kupigwa Faini na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kutolewa nje ya Uwanja na Refa Mark Clattenburg kwenye Mechi waliyotoka 0-0 na Burnley Jumamosi iliyopita Uwanjani Old Trafford.
Jumamosi hiyo, mara baada ya Haftaimu,Mourinho alitolewa kwenye Benchi na kuamriwa kukaa Jukwaa la Watazamaji Uwanjani Old Trafford na Refa Mark Clattenburg baada kuzozana na Refa huyo wakati wa Haftaimu wakielekea kwenye Vyumba vya Kubadili Jezi baada Mourinho kuchukizwa kuwanyima Man United Penati ya wazi pale Matteo Darmian alipoangushwa na Mchezaji wa Burnley Jon Flanagan.

Mbali ya Kifungo cha Mechi 1 ambayo itakuwa Jumapili ijayo Ugenini na Swansea City ambayo sasa ataitazama Jukwaani kwa Watazamaji badala ya kukaa Benchi la Ufundi la Timu yake, Mourinho pia amepigwa Faini Pauni 8,000 kwa Kosa hilo.

Vile vile, kutokana na Kosa lake jingine lililotokana na na matamshi yake kuhusu Refa Anthony Taylor kabla ya Mechi yao na Liverpool mapema Mwezi huu, Mourinho amepigwa Faini ya Pauni 50,000.
Mourinho aliuangalizia kwa mashabiki mpira mechi iliyochezwa hivi karibuni dhidi ya Burnley na kutoka 0-0.