Thursday, November 3, 2016

FIFA BORA 2016: LISTI ZA WAGOMBEA TUZO ZA MAKOCHA BORA ZAWEKWA WAZI

BAADA ya FIFA Jumanne kutangaza Listi ya Wagombea Tuzo ya Kocha Bora kwa Kinamama kwa Mwaka 2016, Jumatano Listi ya Wagombea 10 wa Tuzo ya Kocha Bora 2016 kwa Wanaume ilitangazwa.
Mshindi wa Tuzo hizo mbili atapatikana kwa Kura ambayo Asilimia 50 yake itakuwa ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama wa FIFA na Asilimia 25 nyingine ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki na Asilimia 25 iliyobaki ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.

Majina 10 ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa 2016 kwa Kinamama itatangazwa Leo Alhamisi wakati Listi ya Wachezaji 23 watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa 2016 itaanikwa Ijumaa Novemba 4.

Upigaji Kura wa Tuzo zote za Ubora utaanza Novemba 4 na kufungwa Novemba 22.

Wagombea Watatu wa Mwisho kwa kila Tuzo pamoja na ile Tuzo ya Puskas ya Goli Bora na ile ya Tuzo ya Mashabiki watangazwa Desemba 2.
Image result for The Best Fifa Men's Player 2016
Wagombea 55 wa Timu Bora ya 2016, FIFA FIFPro World11, watatangazwa mwishoni mwa Novemba.

Washindi wa Tuzo hizi za FIFA watatangazwa rasmi Tarehe 9 Januari 2017 kwenye Hafla maalum ya FIFA huko Zurich, Uswisi.

MAKOCHA – WANAUME, Wagombea 10:
* Chris Coleman (Wales/Welsh national team)
* Didier Deschamps (France/French national team)
* Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich/Manchester City)
* Jürgen Klopp (Germany/Liverpool)
* Luis Enrique (Spain/FC Barcelona)
* Mauricio Pochettino (Argentina/Tottenham Hotspur)
* Claudio Ranieri (Italy/Leicester City)
* Fernando Santos (Portugal/Portuguese national team)
* Diego Simeone (Argentina/Atlético Madrid)
* Zinédine Zidane (France/Real Madrid).

MAKOCHA – WANAWAKE, Wagombea 10:

* Philippe Bergeroo (France/French national team)
* Jill Ellis (USA/US national team)
* John Herdman (England/Canadian national team)
* Silvia Neid (Germany/German national team)
* Vera Pauw (Netherlands/South African national team)
* Gérard Prêcheur (France/Olympique Lyonnais)
* Pia Sundhage (Sweden/Swedish national team)
* Oswaldo Vadão (Brazil/Brazilian national team)
* Martina Voss-Tecklenburg (Germany/Swiss national team)
* Thomas Wörle (Germany/FC Bayern Munich).

FIFA – Tuzo za Ubora zitakazotolewa:
-Mchezaji Bora Duniani 2016 [The Best Fifa Men's Player 2016]
-Mchezaji Bora Duniani 2016 kwa Kinamama [The Best Fifa Women's Player 2016]
-Kocha Bora kwa Wanaume 2016 [The Best Fifa Men's Coach 2016]
-Kocha Bora kwa Wanawake 2016 [The Best Fifa Women's Coach 2016]
-Tuzo ya Puskas 2016 kwa Goli Bora [The Fifa Puskas Award 2016 for goal of the year]
-Tuzo ya Uchezaji wa Haki 2016 [The Fifa Fair Play Award 2016]
-Tuzo ya Mashabiki 2016 [The Fifa Fan Award 2016]
-Kikosi Bora 2016 [Fifa FifPro World11]