Thursday, November 24, 2016

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO IPO JUU, LAKINI BRAZIL YAINYEMELEA, TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI 16, NI YA 144

INGAWA Argentina bado ndio Timu Bora Duniani kwa mujibu wa Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo, Brazil, chini ya Kocha wao mpya, inakuja moto na kuinyemelea kwa kasi.
Kwenye Mechi za Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa CONMEBOL, Brazil inaongoza Nchi 10 katika kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia baada ya kushinda Mechi 5 mfululizo chini ya Kocha Tite huku Argentina ikisuasua na kuporomoka hadi Nafasi ya 5 kwenye Kanda hiyo.
Hilo limeifanya Brazil ipande Nafasi 1 kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani na kushika Nafasi ya Pili nyuma ya Argentina huku Mabingwa wa Dunia Germany wakishuka hadi Nafasi ya 3.
England wao wamezidi kushuka, safari hii Nafasi 1, na sasa ni wa 13.
Kwa Afrika Nchi ya Juu kabisa ni Senegal ambayo ipo Nafasi ya 33 wakifuata Mabingwa wa Afrika Ivory Coast ambao ni wa 34 baada kushuka Nafasi 3 lakini wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na wa 36 ni Egypt.
Tanzania ni ya 160 baada ya kuporomoka Nafasi 16 toka Mwezi uliopita walipokuwa Nafasi ya 144.
Listi nyingine ya FIFA ya Ubora Duniani itatolewa Desemba 22.
10 BORA:
1 Argentina
2 Brazil [Imepanda Nafasi 1]
3 Germany [Imeshuka 1]
4 Chile [Imepanda 2]
5 Belgium [Imeshuka 1]
6 Colombia [Imeshuka 1]
7 France
8 Portugal
9 Uruguay
10 Spain