Tuesday, November 22, 2016

FIFA YATANGAZA WAGOMBEA 10 GOLI BORA LA MWAKA!

Leo FIFA imetangaza Magoli 10 Bora kwa Mwaka 2016 ambayo yatapigiwa Kura ili kupata Goli Bora la Mwaka litakaloshinda Tuzo ya Puskas.
Wagombea hawa 10 sasa wanajumuika pia na Wagombea 23 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016 pamoja na Wagombea wengine wa Tuzo mbalimbali zikiwemo za Kocha Bora kwa Waume na Wake na Mchezaji Bora kwa Wanawake.

Magoli hayo 10 yanaweza kuangaliwa kwenye Mitandao ya FIFA FIFA.com/the-best na ule wa FIFA kwenye YouTube.

Magoli haya ni yale yaliyofungwa kuanzia Septemba 2015 hadi Septemba 2016.
Mashabiki wanaweza kupigia Kura Goli wanaloona ni Bora kati ya hayo 10 hadi Desemba 2 na baada ya hapo Magoli 3 Bora yataenda Fainali na Kura kwa Mashabiki zitaanza upya na kuendelea hadi Januari 9 na Mshindi kutangazwa huko Zurich hapo Januari 9, 2017 kwenye Hafla maalum ya kutoa Tuzo za FIFA za Ubora wa Mwaka.

Tuzo ya FIFA ya Puskas ilibuniwa Mwaka 2009 kumuenzi Ferenc Puskás, Nahodha na Staa wa Timu ya Taifa ya Hungary ya Miaka ya 1950.

MAGOLI 10 BORA YA MWAKA:
-Mario Gaspar (Spain) - 13.11.2015, Spain v. England, Kirafiki
-lompho Kekana (South Africa) - 26.03.2016, Cameroon v. South Africa, AFCON
-Marlone (Brazil) - 21.04.2016, Corinthians v. Cobresal, Copa Libertadores
-Lionel Messi (Argentina) - 21.06.2016, USA v. Argentina, Copa América
-Neymar (Brazil) - 08.11.2015, Barcelona v. Villarreal, La Liga (Spain)
-Saúl Ñíguez (Spain) - 27.04.2016, Atlético Madrid v. Bayern Munich, UCL
-Hal Robson-Kanu (Wales) - 01.07.2016, Wales v. Belgium, UEFA EURO 2016
-Daniuska Rodríguez (Venezuela) - 14.03.2016, Venezuela v. Colombia, South American U-17 Women’s Football Championship
-Simon Skrabb (Finland) - 31.10.2015, Gefle v. Åtvidaberg, Ligi Allsvenskan, Sweden
-Mohd Faiz Subri (Malaysia) - 16.02.2016, Penang v. Pahang, Malaysia Super League​