Saturday, November 26, 2016

FULL TIME: BURNLEY 1 v 2 MANCHESTER CITY, AGUERO AIPA USHINDI CITY


MANCHESTER CITY wakicheza Ugenini huko Turf Moor katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuifunga Burnley 2-1 kwa Bao za Sergio Aguero na kukaa kileleni mwa Ligi hiyo.

Dakika ya 14, Mpira mrefu kutoka kwa Kipa wa Burnley Robinson uliokolewa na Sentahafu wa City Otamendi na kutua kwa Dean Marney alieachia kombora la Mita 30 na kuwapa Burnley uongozi.

Dakika ya 37, City walisawazisha kwa Bao la Sergio Aguero alipounganisha Mpira wa Kona.

Kuelekea Dakika za mwisho za Kipindi cha Kwanza, Burnley walipoteza Wachezaji Wawili kwa maumivu pale Mfungaji wao Dean Marney kulazimika kutoka na kuingizwa Arfieldat katika Dakika ya 40 na pia kuingizwa Tarkowskiat kuchukua nafasi ya Gudmundsson kwenye Dakika ya 43.
Hadi Mapumziko, Burnley 1 City 1.
City walifunga Bao lao la Pili Dakika ya 60 Mfungaji akiwa yule yule Sergio Aguero kwa Bao la ngekewa kwani Wachezaji wa Burnley Mee na Stephen Ward waligongana wenyewe wakiwania kuokoa na Mpira kumfikia Fernandinho aliepiga Mpira Goli na kumgonga Sergio Aguero na kutinga.

Matokeo haya yamewaweka City kileleni mwa EPL wakiwa na Pointi 30 kwa Mechi 13 wakifuata Chelsea wenye Pointi 28 kwa Mechi 12 na Liverpool ni wa 3 wakiwa na Pointi 27 kwa Mechi 12.

Chelsea na Liverpool, wanaocheza baadae Leo, wana nafasi ya kuikwanyua City toka kileleni wakishinda hii Leo kwenye Mechi zao.