Thursday, November 3, 2016

KATIBU MSAIDIZI WA KRFA BW. AL-AMIN ABDUL ABDUL AMPONGEZA MWAMUZI JONESIA RUKYAA KUCHEZESHA AFCON YA KINAMAMA

Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera (KRFA), Bw. Al-amin Abdul Abdul amempongeza Mwamuzi wa Kike wa Hapa Kagera Tanzania kwa kuteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), kuwa miongoni mwa waamuzi wa kati 10 watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka huu.
kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika Medani za Kimataifa. 
Jonesia anafanya idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchi za Afrika Mashariki kuwa watano kwani wengine kwa mujibu wa orodha ya CAF ni Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne Wanjala (Kenya) na Suan Ratunga (Burundi). 
Waamuzi wengine ni Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe (Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou (Cameroon) na Aissata Amegee (Togo). Katika orodha hiyo pia yumo Mary Njoroge wa Kenya ambaye mwamuzi wa pembeni pekee. 

Katika fainali hizo, timu shiriki ni Cameroon, Afrika Kusini, Misri na Zimbabwe zipo kundi A wakati Nigeria, Ghana, Kenya na Mali zimo kundi B. 

Jonesia ambaye jana Jumanne alirejea kutoka Cameroon kwenye kozi ya uamuzi ngazi ya juu, kesho Alhamisi anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pale Mtibwa Sugar ya Morogoro itakapokaribishwa na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui. Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbao Fc na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.