Saturday, November 26, 2016

FULL TIME: CHELSEA 2 v 1 TOTTENHAM HOTSPUR, VICTOR MOSES AWAPANDISHA KILELENI BLUES DARAJANI!!

Victor Moses akipongezwa na wenzie baada ya kuwapa bao la pili. Mchezo huo umemalizika kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Tottenham Hotpur kwenye mchezo wa Ligi Kuu England leo Jumamosi, Ligi itaendelea tena kesho jumapili.
Bao za Chelsea zimefungwa na Pedro dakika ya (45') na pili na ushindi liliwekwa kimiani na Victor Moses dakika ya (51') huku bao la Tottenham Hotspur lifungwa na Christian Eriksen dakika ya (11')
Chelsea wamerejea tena kileleni baada ya kuifunga Tottenham 2-1 huko Stamford Bridge.
Kipigo hiki cha Spurs ni cha kwanza kwenye EPL Msimu huu na kufuta ile rekodi yao ya kuwa Timu pekee ambayo ilikuwa haijafungwa kwenye Ligi hiyo inayosifika kuwa ngumu na isiyotabirika Duniani.
Ushindi huo umehakikisha Spurs kutoifunga Chelsea Uwanjani Stamford tangu Februari 1990 na ulikuja kwa Bao la Victor Moses, Mchezaji kutoka Nigeria, aliefunga kwa Shuti la chini katika Dakika ya 51.
Spurs ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 11 kufuatia kazi njema ya Moussa Dembele, Dele Alli na Mpira kumfikia Christian Eriksen alieachia kigongo cha mbali na kutinga.
Christian Eriksen dakika ya (11') aliitangulizia bao Tottenham Hotspur na kuwa 1-0 dhidi ya Wenyeji Chelsea.
JE WAJUA?
-Chelsea hawajafungwa na Tottenham Uwanjani Stamford Bridge katika Mechi 30.

-Mara ya mwisho Chelsea kufungwa Stamford Bridge na Spurs ni Februari 1990.

Chelsea walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Shuti la Pedro na Gemu kwenda Mapumziko ikiwa ni 1-1.

Baada Mechi 13, Chelsea sasa wanaongoza EPL wakiwa na Pointi 31 wakifuata Liverpool na City zenye 30 kila moja na Timu ya 4 ni Arsenal yenye Pointi 25 kwa Mechi 12.

Kesho Jumapili zipo Mechi 4 za EPL lakini macho ni huko Emirates Arsenal wakicheza na Bournemouth na huko Old Trafford wakati Man United wakikipiga na West Ham United.
Image result for Chelsea V Tottenham Hotspur