Saturday, November 5, 2016

FULL TIME EPL: CHELSEA 5 v 0 EVERTON, BLUES WALALA KILELENI!

Bao tano za usiku huu zimeifanya Blues kupanda kileleni kwa kupata pointi 25.
CHELSEA wamekwea kilele cha EPL, Ligi Kuu England, hapo Jana baada ya kuifumua Everton 5-0 huko Stamford Bridge.
Ushindi huu umeifanya Chelsea iongoze EPL ikiwa Pointi 1 mbele ya Man City na Pointi 2 mbele ya Arsenal na Liverpool ambazo zinacheza Leo na zina nafasi za kutwaa uongozi wa EPL wakishinda Mechi zao.
Bao za Chelsea hiyo Jana zilifungwa na Eden Hazard, Bao 2, Alonso, Diego Costa na Pedro.
Hii ni mara ya kwanza kwa Chelsea kutwaa uongozi wa EPL tangu Agosti.