Sunday, November 6, 2016

FULL TIME- EPL...LIVERPOOL 6 v 1 WATFORD, MAJOGOO YAPANDA KILELENI MWA LIGI LEO.

LIVERPOOL Leo wamekwea kilele cha EPL, Ligi Kuu England, baada ya kuitwanga Watford United Bao 6-1 huko Anfield.
Mapema hii Leo Dabi ya London ya Kaskazini ilichezwa huko Emirates kati ya Arsenal na Tottenham na Mechi hii kuwa 1-1 kwa Bao za Kevin Wimmer kujifunga mwenyewe Dakika ya 42 na kuipa Arsenal uongozi wa 1-0 lakini Penati ya Dakika ya 51 iliyotolewa baada Laurent Koscielny kumwangusha Moussa Dembele na kupigwa na Harry Kane iliwapa Spurs Sare.
Watford's Daryl Janmaat scores their first goal Huko Anfield, Bao za Sadio Mane, Bao 2, Coutinho, Emre Can, Firmino na Georginio Wijnaldum ziliwapa Liverpool ushindi mnono wa 6-1 huku Bap pekee la Watford kufungwa na Daryl Janmaat.
 Georginio Wijnaldum of Liverpool scores his sides sixth goal
Ushindi huu umewaweka Liverpool kileleni mwa EPL kwa mara ya kwanza tangu 2014 wakiwa na Pointi 26 wakifuata Chelsea wenye 25 na kisha City na Arsenal wenye 24 huku Spurs wakiwa Watano na Pointi 21 na wa 6 ni Man United wenye 18.
Man United, wakicheza huko Liberty Stadium, waliinyuka Swansea City 3-1 kwa Bao za Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic, Bao 2.
EPL sasa inaenda 'Vakesheni' kupisha Mechi za Kimataifa za Kalenda ya FIFA hadi Jumamosi Novemba 19.Liverpool wanaongoza bao 5-0 mpaka sasa bao zilizofungwa na
Sadio Mané (27', 60')
Philippe Coutinho (30')
Emre Can (43')
Roberto Firmino (57')


Watford bao limefungwa na Daryl Janmaat (75'Liverpool's Sadio Mane celebrates scoring their fifth goal Liverpool's Sadio Mane celebrates scoring their fifth goal Sadio Mane of Liverpool scores his second and his sides fifthLiverpool's Roberto Firmino celebrates scoring their fourth goal