Thursday, November 10, 2016

FULL TIME...VPL: YANGA 1 v 1 RUVU SHOOTING, MSUVA NA NIYONZIMA WAIFUNGIA BAO YANGA LEO.


Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara umekamilika leo kwa Yanga kuitandika Ruvu Shooting mabao 2-1.
Katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru, Mabingwa watetezi Yanga ilipata ushindi kupitia Kia mabao ya Simon Msuva na Haruna Niyonzima.
Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Abdulrahman Musa dakika ya saba kipindi cha kwanza kabla ya Simon Msuva kuisawazishia Yanga dakika 31 baadaye akitumia vyema pasi ya Niyonzima aliyemlamba chenga beki wa Ruvu Shooting.
Yanga waliandika bao la pili na la ushindi dakika ya 57 likifungwa na Niyonzima kwa shuti kali.

Kwa matokeo hayo, sasa Yanga inafikisha ya pointi 33, pointi mbili nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Simba.