Wednesday, November 23, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL 2 v 2 PSG, BARCA NA CITY WAFANYA KWELI

Mechi za 5 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONS, zimemalizika leo Usiku na Timu 2 zaidi, FC Barcelona na Manchester City, kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 usiku huu na  huku wakibakisha Mechi 1 mkononi.

Kwenye Kundi A, Arsenal na Paris St-Germain, ambazo zilikuwa tayari zimeshafuzu, zilipambana huko Emirates Jijini London na hasa kugombea nani atakuwa Mshindi wa Kundi lakini zikatoka Sare ya 2-2 na hivyo kumkosa Mshindi wa Kundi hapo Jana ingawa sasa PSG ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa ushindi huo wa Kundi.

Baada ya Timu hizo kutoka 1-1 huko Paris, Jana Sare ya 2-2 imeipa PSG Bao nyingi za Ugenini na hivyo wana nafasi kubwa kutwaa ushindi wa Kundi wakipata matokeo mazuri kwenye Mechi yao ya mwisho watakayocheza huko kwao na Ludogorets Razgrad, iliyopigwa 6-0 na Arsenal, hapo Desemba 6.

Hapo Jana, PSG walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 18 la Edinson Cavani na Arsenal kujibu kwa Bao 2 za Dakika za 45 na 60 za Olivier Giroud, kwa Penati, na lile la kujifunga mwenyewe Marco Verratti.

Lakini PSG wakasawazisha zikibaki Dakika 13 kupitia Lucas na Gemu kwisha 2-2.
VIKOSI:
Arsenal XI:
Ospina; Jenkinson, Mustafi, Koscielny, Gibbs; Coquelin, Ramsey; Sanchez, Ozil, Iwobi, Giroud
Akiba: Cech, Monreal, Gabriel, Xhaka, Elneny, Oxlade-Chamberlain, Walcott
PSG XI: Areola, Meunier, Marquinhos, Thiago Silva, Maxwell; Verratti, Krychowiak, Motta; Lucas, Cavani, Matuidi
Akiba: Trapp, Kimpembe, Ben Arfa, Jese, Nkunku, Augustin, IkoneTimu 12 ambazo zimefuzu – Bado 4:

-Arsenal, Paris St-Germain, Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Monaco, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Leicester City, Juventus, Barcelona, Manchester City

Timu ambazo zimetupwa nje ya Mashindano:
-Ludogorets, Basel, PSV Eindhoven, FC Rostov, Club Brugge, Dinamo Zagreb, Legia Warsaw, Tottenham, CSKA Moscow, Sporting Lisbon, Dynamo Kiev, Borussia Monchengladbach, Celtic