Sunday, November 27, 2016

FULL TIME: ARSENAL 3 v 1 AFC BOURNEMOUTH, THEO WALCOTT NA ALEXID SANCHEZ WAIPA USHINDI GUNNERS LEO!

Arsenal wakiwa kwao Emirates leo wameshinda Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, kwa kuichapa Bourmouth Bao 3-1 na kuzidi kujichimbia Nafasi ya 4.
Arsenal sasa wana Pointi 28 na juu yao wapo Man City na Liverpool wenye Pointi 30 wakati Vinara Chelsea wana Pointi 31 baada ya Mechi 13 kwa kila Timu.
Arsenal walitangulia kupata Bao baada ya kosa kubwa la Beki wa Bournemouth Steve Cook kutoa pasi fyongo kwa Kipa wake na Alexis Sanchez kuinasa na kufunga kirahisi katika Dakika ya 12.
Bournemouth walirudi kwenye Mechi Refa Mike Jones alipowapa Penati katika Dakika ya 23 kutokana na Nacho Monreal kumwangusha Callum Wilson kwenye Boksi na Wilson kupiga na kufunga Penati hiyo.

Hadi Mapumziko Arsenal 1 Bournemouth 1.
Dakika ya 53, kazi nzuri ya Mesut Ozil na Nacho Monreal ilimfikia Theo Walcott alieipa Arsenal Bao la Pili kwa Kichwa na Bao la 3 kufungwa Dakika ya 91 na Alexis Sanchez alipolishwa na Olivier Giroud.Theo Walcott aliwapachikia bao kwa kichwa na kufanya bao kuwa 2-1 dhidi ya AFC Bournemouth.
Alexis S├ínchez kafunga bao mbili dakika ya  (12', na lile la dakika ya majeruhi la dakika ya 90'+1') huku Theo Walcott akifunga bao dakika ya (53').1-1Sanchez aanza kuifungia Arsenal