Wednesday, November 30, 2016

FULL TIME..EFL CUP: MANCHESTER UNITED 4 v 1 WEST HAM UNITED

MARA baada ya kumalizika Mechi za mwisho za Robo Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi, hapo Jana Droo ya Nusu Fainali ilifanyika na Manchester United kupangwa kucheza na Hull City wakati Liverpool itaivaa Southampton.

Man United, ambayo Jana iliichapa West Ham 4-1 katika Robo Fainali kwa Bao za Zlatan Ibrahimovic na Anthony Martial kila mmoja akifunga 2, watacheza Gemu ya Kwanza ya Nusu Fainali Nyumbani kwao Old Trafford dhidi ya Hull City na kurudiana huko Kingston Communications Stadium.

Kwenye Mechi hiyo, Meneja wa Man United Jose Mourinho hakuwepo kwenye Benchi akiwa anatumikia Kifungo cha Mechi 1 baada kukiri Kosa la kuipiga Teke Chupa ya Maji walipotoka Sare 1-1 na West Ham Jumapili Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
1-0Zlatan Ibrahimovic
Nusu Fainali nyingine, Southampton, ambao Jana waliibwaga Arsenal 2-0 huko, wataanza Nyumbani na kumalizia huko Anfield dhidi ya Liverpool.
Nusu Fainali hizo za Mfumo wa Nyumbani na Ugenini zitachezwa Wiki zinazoanzia Januari kwa Mechi ya Kwanza na ile inayoanzia Januari 23 kwa Mechi za Pili.