Friday, November 18, 2016

MANCHESTER UNITED vs ARSENAL, KESHO JUMAMOSI OLD TRAFFORD: WENGER ASEMA WATAMLINDA MARCUS RASHFORD

Upinzani wa Arsene Wenger na Jose Mourinho ni kitu cha wazi huko England kwa Miaka mingi na Wikiendi hii watakutana tena lakini itakuwa ni mara yao ya kwanza kuvaana tangu Mourinho awe Meneja Mpya wa Manchester United.
Jumamosi Manchester United na Arsenalwatacheza huko Old Trafford Jijini Manchester kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Lakini Wenger amesema tripu hiyo ya Arsenal huko Old Trafford ni Gemu tu kati ya Klabu mbili na si Mameneja Wawili.

Akiongea na Wanahabari hii Leo kuelekea mtanange huu wa Jumamosi, Wenger ameeleza: “Sidhani kama napaswa kuelezea uhusiano wetu. Yeye atapigania Timu yake na mimi nitapigania yangu. Hicho ni kitu cha kawaida!”
Image result for MARCUS RASHFORD
Aliongeza: “Siweki Gemu hizi kama ni Mashindano kati ya Mameneja Wawili. Najua Watu wanataka kutengeneza uhasama lakini hilo halileti Washabiki. Kitu ambacho kinavuta Washabiki ni Gemu yenyewe na ubora wake. Ni muhimu iwe Gemu ya hali ya juu ili kuijengea sifa Ligi Kuu. Hilo ni juu ya Wachezaji Uwanjani.”

Alipoulizwa kama atapeana mkono na Mourinho, Wenger alijibu huku akitabasamu: “Ni wazi kitu hicho. Naheshimu utamaduni huo kwenye Ligi Kuu.”
Kwenye Mechi hii ya Jumamosi, Man United itamkosa Straika wao Zlatan Ibrahimovic ambae yupo Kifungoni Mechi 1 baada ya Kadi za Njano 5 lakini Wenger amemnyooshea kidole Kinda Marcus Rashford ambae kwenye Mechi ya mwisho kati yao, Mwezi Februari, alifunga Bao 2 wakati Man United inaichapa Arsenal 3-2 na kuing’oa kwenye Reli ya kusaka Ubingwa Msimu uliopita.

Wenger amesema: “Mtu alietuua sisi ni Rashford. Hivyo tusidhanie udhaifu wa Man United! Msimu uliopita tulipoteza Gemu 1 tu ya Ugenini, huko Old Trafford. Na hiyo ilikuwa Gemu muhimu kwetu na tukapoteza mwelekeo!”


JE WAJUA?
-Mourinho na Wenger washapambana mara 14 kwenye Ligi Kuu England na Wenger hajashinda hata Mechi 1.

-Mourinho, akiwa na Chelsea, ameibuka Mshindi mara 8 na Sare 6.
-Mara pekee kwa Wenger kumbwaga Mourinho ni Agosti 2015 kwenye Mechi ya kugombea Ngao ya Jamii.