Sunday, November 6, 2016

MANNY PACQUIAO ATWAA MKANDA WA WBO, AMPIGA JESSIE VARGAS JIJINI LAS VEGAS.


Manny Pacquiao akifurahia baada ya kumchapa Jessie Vargas

Arejea na kuondoka na mkanda wa WBO

Pacquiao akipeta baada ya kumwangusha Vargas

Bondia Manny Pacquiao amerejea ulingoni na kupata ushindi wa majaji wote dhidi ya bingwa wa mkanda wa WBO, Jessie Vargas, na kutwaa mkanda huo wa uzito wa welterweight Jijini Las Vegas.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia Pacquiao, 37, alitangaza kujiuzulu masumbwi baada ya kumpiga Timothy Bradley mwezi Aprili.
Katika mchezo wa jana usiky matokeo ya majaji wote watatu yalikuwa ni pointi 114-113, 118-109 na 118-109 yakionyesha Mfilipino Pacquiao ndiye mshindi kwenye pambano hilo.


Bondia Manny Pacquiao akimsukumizia konde la kulia Jessie Vargas

Jassie Vargas akimrushia ngumi ya tumboni Manny Pacquiao

Bingwa wa zamani wa dunia Floyd Mayweather Jr akifuatilia pambano hilo