Tuesday, November 1, 2016

MOURINHO AFUNGULIWA MASHITAKA MENGINE NA FA TENA LEO.


MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amefunguliwa Mashitaka kwa mara ya pili ndani ya Wiki moja na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kutolewa nje ya Uwanja Jumamosi iliyopita Timu yake ilipotoka 0-0 na Burnley huko Old Trafford.
Alhamisi iliyopita, Mourinho alishitakiwa na FA kutokana na matamshi yake kuhusu Refa Anthony Taylor kabla ya Mechi yao na Liverpool mapema Mwezi huu.
Ingawa maneno ya Mourinho kuhusu Refa Taylor hayakuwa mabaya lakini yalivunja Sheria inayokataza Mameneja kuzungumzia Marefa kabla Mechi walizopangiwa na alipewa hadi Jana kujibu Shitaka hilo.
Jumamosi, mara baada ya Haftaimu Mourinho alitolewa kwenye Benchi na kuamriwa kukaa Jukwaa la Watazamaji Uwanjani Old Trafford a Refa Mark Clattenburgbaada kuzozana na Refa huyowakati wa Haftaimu wakielekea kwenye Vyumba vya Kubadili Jezi baada Mourinho kuchukizwa kuwanyima Man United Penati ya wazi pale Matteo Darmian alipoangushwa na Mchezaji wa Burnley Jon Flanagan.
Shitaka hili la limekuja baada ya kupitia Ripoti ya Refa Clattenburg na Mourinho amepewa hadi Ijumaa kujibu Shitaka hili.

Kawaida Adhabu kwa Kosa kama hili ni Onyo, Faini, Kufungiwa kukaa Benchi au Kufungiwa kutokanyaga kabisa Uwanjani.