Tuesday, November 22, 2016

MZAMBIA GEORGE LWANDAMINA ATUA YANGA, MHOLANZI PLUIJM SASA NI MKURUGENZI WA UFUNDI!

MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, Leo wameweka hadharani kuwa Kocha wao mpya kwa ajili ya Mzunguko wa Pili wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, ni George Lwandamina kutoka Zambia lakini aliekuwa Kocha kutoka Uholanzi Hans van de Pluijm atabakia hapo hapo akiwa Mkurugenzi wa Ufundi.
Haya yamethibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga huku akitoboa utambulisho rasmi wa Kocha huyo mpya pamoja na wadhifa mpya wa Pluijm utapangwa.

Mbali ya uthibitisho huo, pia Sanga amesema Kocha Msaidizi Juma Mwambusi atabakia Klabuni hapo.

Lwandamina anategemewa kuanza kazi yake rasmi Novemba 25 wakati Wachezaji watakaporudi Mazoezini kwa ajili ya Mzunguko wa Pili VPL ambao utaanza Desemba 17.