Wednesday, November 16, 2016

NDANI YA OLD TRAFFORD JUMAMOSI MAN UNITED vs ARSENAL, PATA REKODI YA MAMENEJA MOURINHO DHIDI YA WENGER

MTANANGE unaongojewa kwa hamu kati ya Manchester United na Arsenal ambao utachezwa Old Trafford Jijini ManchesterJumamosi hii ikiwa ni Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, utakutanisha Mameneja Wawili ambao ‘hawapendani’.
Hii ni nafasi nyingine kwa uhasama maarufu wa Mameneja Jose Mourinho na Arsene Wenger kujirudia tena, uhasama ambao ulianzia huko London wakati Mourinho akiwa na Chelsea na Wenger na hii hii Arsenal yake.
Hii ni mara ya kwanza kukutana kwao tangu Jose Mourinho atue Man United na hiiitakuwa ni Mechi ya kwanza kwa Timu hizi kupambana Msimu huu

Na mbali ya ‘Vita ya Maneno’ kati yao, ambayo mara nyingi Mourinho huibuka kidedea kwa maneno mafupi na ya kukata maini, hata Uwanjani Mourinho ni kidedea.

Wawili hao washapambana mara 11 kwenye Ligi Kuu England, mara zote Mourinho akiwa na Chelsea na kuibuka Mshindi mara 5 na Sare 6.

Mara pekee kwa Wenger kumbwaga Mourinho ni Agosti 2015 kwenye Mechi ya kugombea Ngao ya Jamii.

Bigi Mechi hii itachezeshwa na Refa Andre Marriner, mwenye Miaka 45, ambaeamesimamia Mechi za Man United za Ligi Kuu England mara 21 Wakishinda 13, Sare 1 na Kufungwa 7 huku akitoa Kadi za Njano 33 na Kadi Nyekundu 1.
Kwa Arsenal, Refa Marriner anakumbukwa sana kwa ajili ya Gemu ya 2014 wakati Chelsea ya Mourinho ikiinyuka Arsenal ya Wenger 6-0 kwa kumpa kimakosa Kadi Nyekundu Kieran Gibbs badala ya Alex Oxlade-Chamberlain.
Baada ya Mechi 11, Liverpool ndio Vinara wakiwa na Pointi 26, Chelsea ni wa Pili wana 25, wakifuata Man City na Arsenal wenye 24 kila mmoja, Tottenham wa 5 wakiwa na 21 na Man United ni wa 6 na wana 18.
Katika Mechi zao za mwisho za EPL kabla hawajapisha Mechi za Kimataifa, Arsenal walitoka 1-1 na Tottenham katika Dabi ya London Kaskazini na Man United kuitandika Swansea 3-1 huko Liberty Stadium, Wales.
Image result for mourinho V wenger
JE WAJUA?
-Tangu Ligi Kuu England ianzishwe Msimu wa 1992/3, Arsenal wameshinda mara 3 tu Old Trafford katika Mechi 24.