Thursday, November 10, 2016

OBAMA NA DONALD TRUMP WAKUTANA USO KWA USO LEO WHITE HOUSE, BARACK OBAMA ASEMA ANAMUUNGA MKONO MTEULE HUYO WA URAIS WA 45 WA MAREKANI BAADA YA KUMWANGUSHA CLINTON!


Rais mteule wa Marekani Donald Trump na rais wa sasa Barrack Obama katika ikulu ya White House

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni ''heshima'' kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.

Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.
Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump 'hafai' kuongoza Marekani.

Hatahivyo Obama alisema kuwa ''anamuunga'' mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.
Baada ya mkutano huo wa ikulu rais Obama alisema kuwa kipaombele chake sasa katika miezi miwili ijayo ni kuhakikisha kuwa kundi litakalosimamia shughuli za mpito linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamezungumza sera za nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba amefurahishwa na maoni ya Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika maswala yanayokabili Marekani.

Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo.
Trump na Obama wakiendelea kuteta jambo White House


Trump akijiachia mbele ya rais Obama

Sasa ni Kazi