Saturday, November 5, 2016

RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII..LEO MAN CITY v MIDDLESBROUGH, CHELSEA v EVERTON. KESHO JUMAPILI ARSENAL v SPURS, SWANSEA v MAN UNITED


EPL - LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Novemba 5 

1800 Bournemouth v Sunderland
1800 Burnley v Crystal Palace
1800 Man City v Middlesbrough
1800 West Ham v Stoke City
2030 Chelsea v Everton

BAADA ya Wiki iliyopita Chelsea kuinyuka Southampton 2-0 wakicheza Ugenini huko Saint Mary na kuchupa hadi Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Vinara Timu 3 zinazofungana kwa Pointi, Man City, Arsenal na Liverpoool, Leo tena Chelsea kwenye EPL, Ligi Kuu England, wako kwao Stamford Bridge kuivaa Everton.

Everton, Timu ambayo ni ngumu na isiyotabirika, wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Chelsea.

Mechi nyingine hii Leo ni huko Etihad Jijini Manchester wakati Vinara wa EPL Man City wakicheza na Middlesbrough, maarufu kama Boro, ambao wako Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Chelsea.

Mechi nyingine hii Leo 3 ambazo Bournemouth wataivaa Sunderland, Burnley kucheza na Crystal Palace na West Ham kuivaa Stoke City.

EPL - LIGI KUU ENGLAND
Jumapili Novemba 6

1500 Arsenal v Tottenham
1715 Hull City v Southampton
1715 Liverpool v Watford
1800 Swansea v Man United
1930 Leicester v West Brom