Tuesday, November 8, 2016

RONALDO NDIYE BORA LA LIGA, AZOA TUZO YA ALFREDO DI STEFANO!

SUPASTAA wa Portugal na Klabu ya Real Madrid ya Spain Cristiano Ronaldo Jana alitunukiwa Tuzo ya Alfredo di Stefano kwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa La Liga.
Ronaldo, ambae pia Jana alithibitisha kusaini Dili Mpya na Real itakayomweka hadi Mwaka 2021, ni mmoja wa Wagombea wa Tuzo nyingine kubwa za Ubora Duniani za Ballon d’Or na ile ya FIFA Mchezaji Bora Duniani ambao Washindi wake watatajwa Desemba na Januari Mwakani.
Ronaldo ametwaa Tuzo ya Alfredo di Stefano inayotolewa na Jardi maarufu huko Spain, Marca, na ambayo inabeba Jina la Lejendari wa Soka wa Spain, baada ya Msimu uliopita kupiga Bao 35 na kutoa Msaada wa Bao 11 katika La Liga Msimu uliopita.

Mwaka huu, Ronaldo amefanikisha Klabu yake Real Madrid kutwaa UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI na Nchi yake Portigal kubeba UEFA EURO 2016 wakiwa ni Mabingwa wa Ulaya.

Akiongea mara baada ya kupokea Tuzo hii, Ronaldo alitamka: “Leo, ni Siku spesho mno kwangu kwa kupata Mkataba Mpya na kupokea Tuzo hii kutoka Marca, nini kingine naweza kuomba?”

“Nina furaha mno. Hii itanipa motisha kufanya kazi kwa bidi na kuboreka zaidi kadri Miaka ikisogea!”