Wednesday, November 16, 2016

SPANEST CUP 2016 YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI IRINGA.


Timu zilizopata nafasi ya kuingia robo Fainali ni pamoja na Kitisi , Nyamahana , makifu mapogoro, Luganga , Itunundu ,Kinyika na Mbugani huku ligi hiyo ikiwa na na kauli mbiu ya “Piga Vita Ujangili Piga Mpira Okoa Tembo”.
Akikabidhi vifaa kwa timu hizo,mratibu wa mashindano hayo alisema kuwa toka kuanza kwa lingi hiyo wananchi wamekuwa wakipewa elimu ya namna ya kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili na kuwa hadi sasa mbali ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali ikiwemo ya baadhi ya timu kuonyesha nidham mbaya wakati wa mechi ila vijana wameonyesha kiwango kikubwa uwanjani
Alizitaja timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na pointi zake katika mabano kwa tarafa ya Idodi kuwa ni Kitisi (12), Nyamahana(6) , makifu (5)na mapogoro(12) wakati tarafa ya Pawaga ni Luganga (14), Itunundu (12),Kinyika(16) na Mbugani (10).
Meng’ataki alisema robo fainali ya kwanza itakuwa na timu za Nyamahana itacheza na timu ya Kitisi kwenye uwanja wa Nyamahana huku Makifu na Mapogolo zitacheza uwanja wa Makifu Novemba 17 mwaka huu , Luganga na Kinyika zitacheza katika uwanja wa Luganga na Itunundu na Mbugani zitacheza uwanja wa Itunundu Novemba 18 mwaka huu .
“Katika robo faina ya pili ya ligi hiyo ya Spanest Cup 2016 Novemba 19 timu ya Kitisi itacheza na Nyamahana katika uwanja wa Kitisi na Mapogolo itacheza na Makifu kwenye uwanja wa Kinyika wakati Novemba 20 itakuwa ni hitimisho ya robo fainali ya pili kwa timu ya Kinyika kucheza na Luganga kwenye uwanja wa Kinyika na Mbugani na Itunundu zitacheza uwanja wa Mbugani na kuwa mechi zote zitaanza kwa wakati na kila timu kuhakikisha saa 9 ;00 Alasiri inakuwepo uwanjani ikiwa imevaa sare kabisa’’’’Alisema Meng’ataki .
Aidha aliongeza kuwa hatua ya nusu fainali itachezwa Novemba 22 na fainali itachezwa Novemba 26 mwaka huu iwapo ratiba hiyo haitavurugika na fainali hiyo itachezwa tarafa ya Idodi .
‘’’’Mshindi wa kwanza atapata kikombe, medali ya dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh 300,000, kutembelea Hifadhi ya Ruaha.Mshindi wa pili atapata medali ya fedha, mipira 2, cheti na Sh 200,000 taslim huku mshindi wa Tatu akipata medali ya shaba, cheti na Sh 100,00 huku mshindi wa nne atazawadiwa Sh 50,000’’’’Alisem,a Meng’ataki

MRATIBU wa mashindano ya SPANEST Cup 2016 Godwell Olle Meing’ataki amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu nane za mpira kati ya 22 zilizoingia robo fainali katika mashindano ya Spanest Cup.
Mratibu wa mashindano ya SPANEST Cup 2016 Godwell Olle Meing’ataki(kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Kiongozi wa timu ya Itunundu Fc Eliopa Maurosi na afisa mtendaji wa kijiji cha Itunundu Halima Kunzugala wakati wa zoezi la kugawa vifaa kwa timu nane kati ya 22 zilizofuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya Spanest Cup 2016.

Baadhi ya viongozi wakiwa katika tukio hilo la ugawaji wa jezi