Sunday, November 6, 2016

TP MAZEMBE WATWAA CAF KOMBE LA SHIRIKISHO, WAIBAMIZA 4 MO BEJAIA!

TP Mazembe ya Congo DR wameiwasha MO Bejaia ya Algeria Bao 4-1 na kutwaa Kombe la Shirikisho kwa jumla ya Bao 5-2 baada ya Mechi 2 za Fainali.
Katika Mechi ya kwanza ya Fainali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Oktoba 29 huko Bilda Nchini Algeria ndani ya Stade Mustapha Tchaker Wenyeji MO Bejaia walitoka Sare 1-1 na TP Mazembe.
Bao za Mechi hiyo zilifungwa kila kipindi na Jonathan Bolingi ndie alieipa TP Mazembe Bao Dakika ya 43 na MO Bejaia kusawazisha Dakika ya 66 Mfungaji akiwa Yaya Faouzi.

Hii Leo huko Lubumbashi, TP Mazembe walitangulia 3-0 kwa Bao za Dakika za 7, 43 na 62 za Bope Merveille na 2 za Rainford Kalaba na MO kupata Bao lao pekee Dakika ya 75 kupitia Morgan Betorangal lakini TP wakapiga la 4 Dakika ya 77 Mfungaji akiwa Jonathan Bolingi.

Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya Mwaka huu kwani zilikuwa Kundi moja ambalo pia Yanga ya Tanzania ilikuwemo na TP Mazembe ndio waliibuka Vinara na MO kushika Nafasi ya Pili huku zikitoka 0-0 huko Algeria na TP Mazembe kushinda 1-0 huko Lubumbashi kwa Bao la Dakika ya 62 la Mzambia Rainford Kalaba.
Hii ni mara ya kwanza kwa TP Mazembe kutwaa CAF Kombe la Shirikisho baada kutwaa CAF CHAMPIONS LIGI mara 5.

Sasa TP Mazembe watakutana na Mabingwa wa CAF CHAMPIONZ LIGI Mamelodi Sundowns kuwania CAF SUPER CUP Mwakani.

VIKOSI:
TP Mazembe:
Gbohouo; Kilitsho, Coulibaly, Luyindama, Mpeko - Bope, Kalaba (Kanda 84'), Adjei (Koffi 77'), Assale - Asante (Adama Traore 69'), Bolingi

MO Bejaia: Rahmani; Benettayeb (Belkacemi 67'), Rahal, Khadir, Sidibe, Athmani, Betorangal, Baouali, Salhi, Ferhat (Yesli 61') - Yaya