Sunday, November 13, 2016

TUZO YA BBC MCHEZAJI BORA WA AFRIKA WA MWAKA: 5 WAGOMBEA!

Image result for Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya TourePierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Yaya Toure

Ndio Wagombea Watano watakaoingia Fainali ya kuwania Tuzo maarufu ya BBC ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka.

Mshindi wa Tuzo hii ataamuliwa kwa Kura za Mashabiki wa Soka Duniani kote ambazo watapiga Mtandaoni kwenye Tovuti ya BBC, Shirika la Utangazi la Uingereza.

Mashabiki wamepewa hadi Saa 3 Usiku Novemba 28 kupiga Kura yao na Mshindi kutagazwa Desemba 12 kuanzia Saa 2 Dakika 35 Usiku.

Kwa Straika wa Borussia Dortmund na Gabon Aubameyang hii itakuwa ni mara yake ya 4 mfululizo kutinga Fainali kuwania Tuzo hii wakati Mchezaji wa Ghana na West Ham, Andre Ayew, ambae aliishinda Tuzo hii Mwaka 2011, ni mara yake ya 4 kufika Fainali.

Kwa Riyad Mahrez, Fowadi wa Algeria na Klabu Bingwa ya England Leicester City, hii ni mara yake ya kwanza kabisa kuwemo kwenye kinyang’anyiro hiki wakati Straika wa Liverpool na Senegal, Sadio Mane, hii ni mara yake ya pili kuwemo baada ya Mwaka Jana pia kuwa Mgombea kwenye Fainali.

Kiungo wa Ivory Coast, Yaya Toure, ambae ameizoa Tuzo hii mara 2, hii ni mara yake ya 8 mfululizo kuwa Mgombea.

WASIFU WA WAGOMBEA:
Pierre-Emerick Aubameyang

Aubameyang, Mwenye Miaka 27, ameng’ara sana Mwaka huu 2016 akifunga Bao 26 kwa Klabu yake Borussia Dortmund hadi sasa.

Yeye amekuwa Mwafrika wa Kwanza kutajwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa Bundesliga huko Germany na pia ni Mchezaji wa Kwanza kutoka Gabon kutwaa Tuzo ya CAF ya Mchezaji Bora wa Mwaka.

Mwaka huu, Aubameyang, yupo kwenye Listi ya Wagombea wa Tuzo ya 2016 Ballon d'Or.

Andre Ayew
Mwezi Agosti, Ayew alivunja Rekodi ya kununuliwa kwa Dau kubwa na Klabu ya West Ham walipoilipa Swansea Pauni Milioni 20.5 kumnunua.

Akiwa na Swansea, aliipigia Bao 12 katika Mechi 35 na kuzoa Tuzo ya Klabu hiyo ya Mchezaji Mpya Bora.

Riyad Mahrez
Msimu uliopita, ulioisha Mwezi Mei Mwaka huu, Mahrez ndie alitwaa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England na kuwa Mwafrika wa Kwanza kuizoa.

Mahrez, mwenye Miaka 25, aliifungia Leicester Bao 17 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa England.

Sadio Mane
Mane, mwenye Miaka 24, ameweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa Bei ghali kutoka Afrika pale Liverpool ilipomnunua kwa Dau la Pauni Milioni 34 mwanzoni mwa Msimu huu.

Alipotua tu Liverpool, Mane alifunga Bao 6 na kutoa Msaada wa Magoli mara 4 katika Mechi zake 11 na kabla, akiwa na Southampton mwanzoni mwa Mwaka huu, aliifungia Timu hiyo Bao 8 ikiwemo Hetitriki dhidi ya Man City.

Yaya Toure
Toure, mwenye Miaka 33, Mwezi Februari alitwaa Taji lake la 17 alipoisaidia Man City kubeba Kombe la Ligi walipoifunga Liverpool kwa Mikwaju ya Penati nay eye ndie aliefunga Penati ya ushindi.

KWA KUPIGA KURA INGIA TOVUTI YA BBC: http://www.bbc.com/sport/football/37925428