Tuesday, November 1, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO ARSENAL, PSG ZAWANIA KUFUZU ZIKIWA NA MECHI 2 MKONONI!

LEO Mechi za 4 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, zitaanza kuchezwa na kwenye Kundi A Arsenal na Paris Saint-Germain zipo kileleni zikiwa zimefungana kwa Pointi na zote Leo hii zina nafasi nzuri sana kufuzu hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakibakisha Mechi 2 mkononi.
Arsenal hii Leo wapo Ugenini huko Bulgaria kucheza na Ludogorets Razgrad ambayo waliipiga 6-0 Mwezi uliopita huko Emirates wakati PSG wapo pia Ugenini huko Uswisi kurudiana na FC Basel waliyoitandika 3-0 huko Paris, France Mwezi uliopita.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Ratiba
Mechi za 4 za Makundi
Saa 4 Dakika 45 Usiku huu

Jumanne Novemba 1
KUNDI A

Basel v Paris St Germain
Ludogorets Razgrad v Arsenal
KUNDI B
2045 Besiktas v Napoli
Benfica v Dynamo Kiev
KUNDI C
Borussia Monchengladbach v Celtic
Man City v Barcelona
KUNDI D
Atletico Madrid v FC Rostov
PSV Eindhoven v Bayern Munich