Thursday, November 3, 2016

UEFA EUROPA LEAGUE LIVE: FENERBAHCE 2 vs 0 MANCHESTER UNITED

Jeremain Lens kipindi cha pili dakika ya (59') aliwaongezea bao la pili na kufanya Fenerbahce kuongoza 2-0 dhidi ya Timu ya England Manchester United kwenye Kombe la Uefa Europa League.

Zlatan Ibrahimovic aliingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Pogba kwa Manchester United katika kipindi cha kwanza.Pogba akitoka uwanjani baada ya kuumia mguuBao la mapema la Moussa Sow dakika ya 2 limewatoa mchezoni Man United na huku wakionekana kuzidiwa United huku Staa wao Pogba akiumia na kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahimovic dakika ya 30 kipindi cha kwanza.1-0 dakika ya 2 tu Fenerbahce Moussa Sow kawachungulia Man United dakika ya 2 na sasa ni dakika 22 bao ni 1-0 kipindi cha pili.Zlatan Ibrahimovic at Man United training
Man United wajiuliza dhidi ya Fenerbahce.
VIKOSI:
Fenerbahce:
Demirel, Ozbayrakli, Skrtel, Kjaer, Kaldirim, Souza, Potuk, Topal, Lens, Sow, Sen
Fenerbahce Akiba: Fabiano, Van Persie, Koybasi, Emenike, Neustadter, Ucan, Stoch
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Rojo, Blind, Shaw, Schneiderlin, Ander Herrera, Rashford, Pogba (Ibrahimovic), Martial, Rooney
Man Utd Akiba: Romero, Jones, Mata, Young, Mkhitaryan, Fellaini

MANCHESTER UNITED Usiku huu wapo huko Uwanja wa Fenerbahce Sukru Saracoglu Jijini Instanbul Nchini Turkey kupambana na Fenerbahce katika Mechi ya Marudiano ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Old Trafford Wiki 2 zilizopita, Man United waliitandika Feberbahce Bao 4-1 kwa Bao za Pogba, Bao 2, Lingard na Marial wakati la Fenerbahce lilifungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United Robin van Persie.
Hii itakuwa ni Mechi ya 4 ya Kundi A ambalo Feyenoord na Man United wapo kileleni wote wakiwa na Pointi 6 na wa 3 ni Fenerbahce wenye 4 na Zorya Luhansk wapo mkiani wakiwa na Pointi 1 tu.