Thursday, November 3, 2016

UEFA EUROPA LEAGUE: FENERBAHCE 2 vs 1 MANCHESTER UNITED, UNITED HOI UTURUKI!!! IBRA CHUPUCHUPU AONESHWE KADI NYEKUNDU!

Bao la kufutia machozi lilifungwa na Nahodha Wayne Rooney dakika ya 89 na mtanange kumalizika kwa bao 2-1.
Timu ya Fenerbahce imefunga mara mbili magoli mazuri dhidi ya Manchester United na kukifanya kikosi hicho cha Jose Mourinho kuwa hatarini kuondolewa katika Ligi ya Uropa.
Mshambuliaji Moussa Sow aliipatia Fenerbahce goli la kuongoza katika sekunde ya 65 kwa kufunga kwa tik taka na kisha Jeremain Lens kufunga goli la pili la mpira wa adhabu.

Katika mchezo huo Manchester United ilishuhudia Paul Pogba alitoka nje baada ya kuumia, hata hivyo baadaye Wayne Rooney alifunga goli pekee kwa timu yake kwa shuti la yadi 25.

Moussa Sow akifunga goli la kwanza katika mchezo huo kwa tik taka

Jeremain Lens akishangilia goli lake alilofunga kwa kukimbia
Manchester United suffer more woe: Moussa Sow and Jeremain Lens pile misery on Jose2-0 kabla ya mtanange kumalizika.......Rooney akiteta jambo na Ibra
Jeremain Lens kipindi cha pili dakika ya (59') aliwaongezea bao la pili na kufanya Fenerbahce kuongoza 2-0 dhidi ya Timu ya England Manchester United kwenye Kombe la Uefa Europa League.

Zlatan Ibrahimovic aliingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Pogba kwa Manchester United katika kipindi cha kwanza.Pogba akitoka uwanjani baada ya kuumia mguuBao la mapema la Moussa Sow dakika ya 2 limewatoa mchezoni Man United na huku wakionekana kuzidiwa United huku Staa wao Pogba akiumia na kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahimovic dakika ya 30 kipindi cha kwanza.1-0 dakika ya 2 tu Fenerbahce Moussa Sow kawachungulia Man United dakika ya 2 na sasa ni dakika 22 bao ni 1-0 kipindi cha pili.Zlatan Ibrahimovic at Man United training
Man United wajiuliza dhidi ya Fenerbahce.
VIKOSI:
Fenerbahce:
Demirel, Ozbayrakli, Skrtel, Kjaer, Kaldirim, Souza, Potuk, Topal, Lens, Sow, Sen
Fenerbahce Akiba: Fabiano, Van Persie, Koybasi, Emenike, Neustadter, Ucan, Stoch
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Rojo, Blind, Shaw, Schneiderlin, Ander Herrera, Rashford, Pogba (Ibrahimovic), Martial, Rooney
Man Utd Akiba: Romero, Jones, Mata, Young, Mkhitaryan, Fellaini

MANCHESTER UNITED Usiku huu wapo huko Uwanja wa Fenerbahce Sukru Saracoglu Jijini Instanbul Nchini Turkey kupambana na Fenerbahce katika Mechi ya Marudiano ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Old Trafford Wiki 2 zilizopita, Man United waliitandika Feberbahce Bao 4-1 kwa Bao za Pogba, Bao 2, Lingard na Marial wakati la Fenerbahce lilifungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United Robin van Persie.
Hii itakuwa ni Mechi ya 4 ya Kundi A ambalo Feyenoord na Man United wapo kileleni wote wakiwa na Pointi 6 na wa 3 ni Fenerbahce wenye 4 na Zorya Luhansk wapo mkiani wakiwa na Pointi 1 tu.