Thursday, November 3, 2016

UEFA EUROPA LIGI: LEO UTURUKI FENERBAHCE vs MAN UNITED

MANCHESTER UNITED Usiku huu wapo huko Uwanja wa Fenerbahce Sukru Saracoglu Jijini Instanbul Nchini Turkey kupambana na Fenerbahce katika Mechi ya Marudiano ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Old Trafford Wiki 2 zilizopita, Man United waliitandika Feberbahce Bao 4-1 kwa Bao za Pogba, Bao 2, Lingard na Marial wakati la Fenerbahce lilifungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United Robin van Persie.
Hii itakuwa ni Mechi ya 4 ya Kundi A ambalo Feyenoord na Man United wapo kileleni wote wakiwa na Pointi 6 na wa 3 ni Fenerbahce wenye 4 na Zorya Luhansk wapo mkiani wakiwa na Pointi 1 tu.

Huenda kwenye Mechi hii Meneja wa Man United Jose Mourinho akamtumia Henrikh Mkhitaryan ambae hajacheza tangu Septemba pamoja na Anthony Martial, Timothy Fosu-Mensah na Phil Jones ambae hajacheza tangu aumie Januari.

Lakini itawakosa Antonio Valencia, alievunjika mkono, Chris Smalling, Michael Carrick na Memphis Deepay ambao hawamo kwenye Kikosi cha huko Uturuki.