Sunday, November 6, 2016

FULL TIME: KAGERA SUGAR 2 vs 1 RUVU SHOOTING, TEMI FELIX, MANGOMA NA MBARAKA WAIPANDISHA KAGERA NAFASI YA TATU!


Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusup bao la tatu leo kwenye mtanange wa VPL uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kagera Sugar wamepanda juu nafasi ya Tatu kwenye Msimamo wa VPL baada ya kuwanyuka bao 3-1 Timu ya Ruvu Shooting.
Bao la kwanza la Kagera na la kusawazisha limefungwa na Temi Felix kipindi cha pili baada ya kuongeza kasi, Bao alilolifunga kwa shuti kali kwa mpira wa adhabu. Bao la pili lilifungwa na Seleman Mangoma na la tatu likafungwa na Mbaraka Yusuf. 
Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Sehemu ya Benchi la Timu ya Kagera Sugar.
Mbaraka Yusuf alikunjuka zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika na kumchambua beki wa Ruvu Shooting na kuziona nyavu za Ruvu Rooting ambapo mpaka wakati huo Kipa hakuwepo langoni mwake. Ushindi huo wa Kagera Sugar umewapandisha juu nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24. Ligi hii ya Vodacom sasa inaenda mapumziko ya msimu wa kwanza wa 2016/2017.
Kipindi cha pili Tem Felix aliisawazishia bao Kagera Sugar na Kisha baadae Seleman Mangoma akapachika bao la pili na kufanya Kagera Sugar waongoze kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting.Seleman Mangoma Kulia baada ya kuziona nyavu za Ruvu Shooting leoBaadhi ya Wachezaji wa Ruvu Shooting wakipongezana baada ya kuwafunga bao Kagera Sugar dakika ya 45 mwishoni mwa kipindi cha kwanza jioni hii jumapili.
Said Dunga dakika ya 45 kipindi cha kwanza aliifungia bao RUVU SHOOTING na kwenda mapumziko wakiongoza bao 1-0 dhidi ya 
wenyeji Kagera Sugar.

Waamuzi wa Mtanange  kati ya Kagera Sugar V Ruvu Shooting wakati wa mapumziko wakitoka Nje ya Uwanja kwenda kwenye mapumziko ya dakika chache kujiandaa na dakika 45 za kipindi cha pili. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Benchi la Timu ya Ruvu Shooting wakishangilia bao kipindi cha kwanza mwishoni dakika ya 45 na kwenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0.