Sunday, November 20, 2016

WAYNE ROONEY AKERWA NA KUSAKAMWA ENGLAND!

Wayne Rooney amedai amekuwa akisakamwa mno wakati akiichezea England na hilo ni tendo la fedheha kubwa.
Rooney ameichezea England Mechi 119 akiwa ni wa pili katika Historia kwa kucheza Mechi nyingi nyuma ya Kipa Peter Shilton aliecheza Mechi 125 na pia ndie Mfungaji Bora katika Historia ya Nchi hiyo.
Hivi karibuni Jarida moja huko England lilitoa Picha za Rooney akinywa Pombe Hotelini waliyokuwa wakikaa Timu ya England ingawa Siku hiyo Kikosi chote kilikuwa kimepewa Ofu na Meneja Gareth Southgate.
Akiongea hapo Jana mara baada ya Mechi ya Man United na Arsenal, Rooney aliwashambulia wanaomsakama na kudai wanakosa heshima.
Alisema: "Inaonyesha kama Wanahabari wanaandika Wasifu wa Kifo changu na hilo sitaruhusu litokee. Yanayotokea ni fedheha. Napenda kuchezea Nchi yangu na naskia fahari mafanikio yangu. Bado sijaisha!"
Nao Wachezaji wa zamani wa England, Ian Wright na Alan Shearer, wamejitokeza kumpa sapoti Rooney.
Akiongea hapo Jana, Ian Wright, alisema: "Kwa Miaka Mitatu au Minne wamekuwa wakimshambulia. Nimefurahi mno sasa anajibu mapigo. Pigana Wayne!"
Nae Nahodha wa zamani wa England Alan Sherer amesema: "Siku zote amejitolea kwa nguvu zote kuichezea England. Kama alipewa Ofu na kuamua kubaki Hotelini na kupata kinywaji hakufanya kosa labda ingekuwa ameenda kinyume na Meneja!"