Sunday, November 13, 2016

WAZIRI WA MICHEZO ARIDHISHWA NA UKARABATI UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA. KAMPUNI YA MAFUTA MOIL YAONESHA NIA YA KUWEKA MAJUKWAA


Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua. Waziri Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa miguu.