Sunday, November 20, 2016

YAYA TOURE ARUDI MAN CITY NA KUIPATIA USHINDI TIMU HIYO, PEP ASHANGAA NA KUDUWAA!

Mara baada ya Jana kuchezeshwa kwa mara ya kwanza baada Miezi Mitatu baada kupigwa stopu na Meneja Pep Guardiola kufuatia ugomvi na Wakala wake, Yaya Toure ambae alifunga Bao zote 2 wakati Man City inaifunga Crystal Palace 2-1 amefunguka na kusema hakushangazwa kuitwa kuichezea tena Timu hiyo.
Toure, mwenye Miaka 33, ameeleza: "Nilikuwa tayari kiakili na nilijua ipo Siku Meneja ataniita!"

Toure, ambae ameiwezesha City kutwaa Ubingwa EPL mara 2, Jana alipokewa vizuri na Mashabiki wa Timu hiyo waliokuwa wakimuimba Mechi nzima.
Mwishoni mwa Mechi hiyo na Palace Wachezaji wote wa City walimshangilia Toure na kumsindikiza kwa Makofi hadi nje ya Uwanja.