Saturday, December 24, 2016

CRYSTAL PALACE YAMTEUA BIG SAM KUWA MENEJA MPYA LEO

Crystal Palace wamemteua Sam Allardyce kuwa Meneja wao mpya baada ya kumtimua Alan Pardew.
Pardew, ambae alikuwa Palace tangu Januari 2015, alitimuliwa Alhamisi akiiacha Timu ikiwa Nafasi ya 17 kwenye EPL, Ligi Kuu Vodacom.
Mechi ya kwanza kwa Sam Allardyce itakuwa Jumatatu Ugenini na Watford.
Akiongea baada ya uteuzi wake, Allardyce amesema: "Natumai tutaleta furaha hasa kipindi hiki cha Krismasi na Mswaka Mpya na pia kwa muda mrefu!”
Allardyce amekuwa hana kazi tangu mwishoni mwa Septemba baada ya kuacha kazi ya Umeneja wa Timu ya Taifa ya England alikokaa kwa Siku 67 tu.