Thursday, December 22, 2016

CRYSTAL PALACE YAMTIMUA MENEJA ALAN PARDEW, BIG SAM KUSHIKA MIKOBA YAKE!

https://pbs.twimg.com/media/C0SiwKiWgAA9ZEt.jpg:smallCRYSTAL PALACE imemtimua kazini Meneja wao Alan Pardew na taarifa zilizovuja ni kuwa Sam Allardyce ataingia mazungumzoni kushika wadhifa huo.
Pardew, mwenye Miaka 55, anaiacha Palace ikiwa Nafasi ya 17 kati Msimamo wa Timu 20 za EPL, Ligi Kuu England.
Jumamosi iliyopita Palace walifungwa 1-0 na Vinara Chelsea na kabla yah apo walichapwa na Manchester United.
Crystal Palace wako Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo ndio huporiomoka Daraja na hali hii imekuja licha ya kutumia Dau kubwa kununua Wachezaji akiwemo Straika wa Ubelgiji Christian Benteke waliemlipia Pauni Milioni 32 kumnunua.
Inaaminika Meneja aliepita wa England, Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, atafanya mazungumozo na Bodi ya Palace ndani ya Masaa 24 yajayo.
Mechi ifuatayo kwa Palace ni Siku ya Boksingi Dei, Desemba 26, ambapo Palace watacheza na Watford kwenye EPL.