Monday, December 26, 2016

EPL – BOXING DAY: LEO MAN UNITED v SUNDERLAND, MOYES ANAREJEA OLD TRAFFORD

LEO katika Moja ya Mechi 8 za EPL, Ligi Kuu England,ni ile itakayochezwa huko Old Trafford kati ya Manchester United na Sunderland na mvuto mkubwa ni kurejea tena Uwanjani hapo kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.
Mwenyewe Moyes ameshakiri kuwa ni kitu kisichowezekana kuendeleza urithi wa Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.
Lakini Meneja wa sasa wa Man United, Jose Mourinho, ametoboa anafurahia changamoto hizo na hataruhusu presha zimshinde.

Akiongea kuelekeaechi hii ya Leo, Mourinho ameeleza: “Sioni kama ni mzigo. Nahisi Historia kubwa ya Klabu hii ni kitu kizuri na siwazii mabaya. Tatizo ukipewa masharti ya kufuata!”
Alipoulizwa kama Moyes ndie alikuwa na changamoto kubwa kwani ndie alierithi moja kwa moja toka kwa Ferguson, Mourinho alijibu: “Sitajali kuwa kwenye Klabu yenye matumaini makubwa lakini kuwa nao Ryan Giggs, Nemanja Vidic, Patrice Evra na Chicharito kwenye Timu. Hilo sijali hata kidogo!” Tahmini
Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi 4 mfululizo katika Mashindano yote na kuzoa Pointi 9 kati ya 9 kwenye EPL.
Sunderland, walioanza Msimu vibaya, walijikongoja Mwezi Novemba wakishinda Mechi 2 kati ya 3 na Mwezi huu walishinda Mechi zao 2 za Nyumbani dhidi ya Leicester na Watford na kuleta matumaini mapya.

Wakati Man United wapo Nafasi ya 6, Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tottenham na 4 nyuma ya Arsenal ambao ni wa 4, Sunderland wapo Nafasi ya 18 wakiwemo kwenye zile 3 za Mkiani ambazo hushuka Daraja mwishoni mwa Msimu.

Msimu uliopita:

Man United waliichapa Sunderland 3-0 Uwanjani Old Trafford kwa Bao za Wayne Rooney, Memphis Depay na Juan Mata na kufungwa 2-1 huko Stadium of Light..


EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace
1800 Arsenal v West Bromwich Albion
1800 Burnley v Middlesbrough
1800 Chelsea v Bournemouth
1800 Leicester City v Everton
1800 Manchester United v Sunderland
1800 Swansea City v West Ham United
2015 Hull City v Manchester City