Saturday, December 31, 2016

EPL FUNGA MWAKA MECHI YA KUKATA NA SHOKA LEO ANFIELD, LIVERPOOL vs MAN CITY

Video thumbnail, Liverpool vs Man City - Match PreviewLigi Kuu England Inaendelea tena leo Jumamosi, Chelsea Vinara wa Ligi hiyo wakiwa na hakika ya kumaliza Mwaka huu 2016 wakiongoza Ligi, vita kubwa ipo huko Anfield hii Leo ambako Liverpool wanapambana na Manchester City kuwania nani atafunga Mwaka akiwa Nafasi ya Pili.
Chelsea wapo kileleni wakiwa na Pointi 46, Liverpool wanafuata wakiwa na Pointi 40 na City ni wa 3 wakiwa na Pointi 39.

Leo Chelsea watacheza mapema kwao Stamford Bridge na Stoke City na kuacha zigo kubwa kwa Liverpool na Man City kupigana baadae Usiku.

Kitu chema kwa City ni kurejea tena dimbani kwa Straika wao mkuu Sergio Aguero aliyekuwa Kifungoni kwa Mechi 4.

Lakini Klabu zote zina Majeruhi kadhaa na kwa Liverpool hao ni Grujic, Coutinho, Matip, Bogdan na Ings wakati wa City ni Kompany, Delph na G√ľndogan.

Kwenye Mechi kama hii iliyochezwa Anfield Msimu uliopita Last season Liverpool 3 Manchester City 0.

Nini Mameneja Wameongea?

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp: "Hii ni Gemu kubwa kwa kila Timu. Klabu 6 zinagombea Nafasi 4 au moja. Kila Gemu ni kama Fainali.”

“City wana vipaji kwenye Timu yao na Benchi lao. Kitu cha maana kwetu ni kuchezea Anfield. Ni lazima tutumie hilo!” Meneja wa Manchester City Pep Guardiola: "Wao ni Wagombea Ubingwa. Nishawahi kucheza dhidi ya Jurgen Klopp, tunajuana. Anfield itawapa matumaini makubwa!”