Saturday, December 31, 2016

EPL: HULL CITY 2 vs 2 EVERTON

Everton walisawazisha Dakika ya 84 kwa Bao la Ross Barkley na kupata Sare ya 2-2 walipocheza na Hull City huko Kingston Communications Stadium kwenye Mechi pekee Jana Usiku ya EPL, Ligi Kuu England.
Matoke ambayo yamewatoa Hull kutoka mkiani na sasa wapo Nafasi ya 19 huku Everton wakibakia Nafasi yao ile ile ya 7.
Hull walitangulia kufunga kwa Bao la Michael Dawson na Everton kusawazisha Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza baada ya Kipa David Marshall kupanchi Mpira wa Kona ya Kevin Mirallas na kutumbukia wavuni.

Frikiki ya Robert Snodgrass iliwapa Hull uongozi wa 2-1 lakini Barkley akawapa Sare ya 2-2.

Leo zipo Mechi 7 za EPL za kufunga Mwaka nay a mwisho kabisa ni ule Mtanange mkali huko Anfield kati ya Liverpool na Manchester City.