Sunday, December 4, 2016

EPL: AFC BOURNEMOUTH 4 vs 3 LIVERPOOL, MAJOGOO YABANWA MBAVU UGENINI!!

LEO kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, huko Fitness Stadium Wenyeji Bournemouth walitanguliwa 2-0 na Liverpool hadi Mapumziko lakini wakaibuka na kushinda 4-3.
Liverpool walifunga Bao zao 2 a kwanza kupitia Sadio Mane na Divock Origi kabla Haftaimu na Bournemouth kupata Penati na kufunga Dakika ya 56.
Lakini Liverpool wakaebda 3-1 mbele kwa Bao la Emre Can.
Bournemouth wakapiga Bao lao la Pili kupitia Fraser Dakika ya 76 na Dakika 2 baadae Gemu kuwa 3-3 kwa Bao la Cook.

Bao la 4 na la ushindi Dakika ya 93 Mfungaji akiwa Nathan Ake.