Saturday, December 3, 2016

FULL TIME: MANCHESTER CITY 1 vs 3 CHELSEA

VINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Leo wamezidi kupeta kileleni sasa wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Liverpool baada kutoka nyuma kwa Bao 1 na kuilaza Manchester City 3-1.
Hadi mapumziko City walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Chelsea kujifunga wenyewe wakati Beki Gary Cahill alipoukwamisha wavuni katika Dakika ya 45.
Chelsea walisawazisha Bao hilo Dakika ya 60 kupitia Diego Costa.
Wilian aliwapeleka Chelsea 2-1 mbele kwa Bao la Dakika ya 70 na Dakika ya 90 Eden Hazard kuwapa Chelsea Bao la 3.
Katika Dakika za Majeruhi Fowadi wa City Sergio Aguero alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya David Luis na tukio lilifanya zitokee rabsha miongoni mwa Wachezaji wa Timu zote 2 na kusababisha Fernandinho wa City nae kupewa Kadi Nyekundu.
Wakati Fernandinho atafungiwa Mechi 3 ipo hatari Aguero akafungiwa Mechi 4 au zaidi kwa vile alishawahi kufungiwa Mechi 3 huko nyuma.