Saturday, December 10, 2016

EPL - ARSENAL 3 vs 1 STOKE CITY, OZIL AITAWANYA STOKE EMIRATES NA KUIPANDISHA KILELENI!

Wenyeji Arsenal walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Stoke Bao 3-1 na kuishika Chelsea kileleni mwa EPL wote wakiwa na Pointi 34 lakini Arsenal wako juu kwa Ubora wa Magoli.
Arsenal walilazimika kumuingiza Hector Bellerin Dakika ya 25 kumbadili Mustafi alieumia.
Stoke walifunga Bao lao kwa Penati ya Kepteni wao Charlie Adam iliyotolewa na Refa Lee Mason kufuatia Granit Xhaka kumpiga Kipepsi Joe Allen bila kupewa Kadi yeyote mbali ya kutolewa hiyo Penati.

Theo Walcott aliirudisha Arsenal kwenye Gemu kufuatia Bao lake safi la Dakika ya 42 alipounganisha Pasi ya Bellerin.
Hadi Haftaimu Arsenal 1 Stoke 1.
Kipindi cha Pili Arsenal walifunga Bao 2 nyingine kwenye Dakika za 49 na 75 Wafungaji wakiwa Mesut Ozil na Iwobi.
Ozil aipa Arsenal bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Stoke CityArsenal