Sunday, December 11, 2016

FULL TIME: REAL MADRID 3 v 2 DEPORTIVO LA CORUNA, SERGIO RAMOS AIPA USHINDI REAL DAKIKA ZA MAJERUHI!

SERGIO RAMOS tena alifunga Bao muhimu katika Dakika za lala salama na kuipa ushindi Real Madrid wa Bao 3-2 walipocheza na Deportivo La Coruna ambao umewafanya wawe juuu kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Barcelona.
Mapema Jana, Barca waliichapa Osasuna 3-0. 

Real, wakicheza kwao Santiago Bernabeu bila Cristiana Ronaldo, walikuwa 2-1 nyuma na kusawazisha na kushinda katika Dakika 6 za mwisho kwa Bao za Morata, Dakika ya 50, Mariano, Dakika ya 84 na Ramos Dakika ya 92.
Bao za Deportivo zilifungwa na Joselu Dakika za 63 na 65.
Ushindi huo pia umeweka Rekodi mpya kwa Klabu ya Real ya kutofungwa katika Mechi 35.
Sasa Real wanaruka kwenda Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.