Sunday, December 25, 2016

JOSE MOURINHO ASEMA KWA SASA ANAJISIKIA YUPO NYUMBANI OLD TRAFFORD!

Jose Mourinho ameeleza kuwa sasa yupo na furaha akiwa na Manchester United na imekuwa rahisi kwake kujisikia Nyumbani kwa Klabu hiyo ambayo ni moja ya Klabu kubwa Duniani.

Mourinho, ambae ametua Man United mwanzoni mwa Msimu huu, alianza vizuri kwenye EPL, Ligi Kuu England, lakini baadae wakayumba na sasa wamerudi kwenye Reli na wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tootenham, Pointi 4 nyuma ya Arsenal walio Nafasi ya 4, Pointi 6 nyuma ya City ambao ni wa 3, Pointi 7 nyuma yaw a 2 Liverool na 13 nyuma ya Vinara Chelsea.
Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Jumatatu na Sunderland, Mourinho amesema: “Watu wanataka kuwa na furaha tena…Watu wana matumaini makubwa ingawa kwa sasa hatupo nafasi nzuri!”
Jose Mourinho ameeleza kuwa sasa yupo na furaha akiwa na Manchester United na imekuwa rahisi kwake kujisikia Nyumbani kwa Klabu hiyo ambayo ni moja ya Klabu kubwa Duniani. Jumatatu, Uwanjani Old Trafford, Man United itacheza na Sunderland ambayo iko Nafasi ya 18 na wapo chini ya Meneja wa zamani wa Man United David Moyes ambae alimrithi Lejendari Sir Alex Ferguson Mwaka 2013 na kutimuliwa Miezi kadhaa baadae.

Mourinho, ambae sasa ameiongoza Man United kwenye Mechi 10 bila kufungwa, ametoboa kuwa hajawahi kuongea na Moyes.

Mourinho pia aliponda Ratiba ya EPL kwa kipindi hiki cha Krismasi na Mwaka Mpya na kudai baadhi ya Klabu zimependelewa.

Ameeleza: “Kipindi hiki kigumu cha Mechi mfululizo, Chelsea wako na Ratiba nyepesi isiyokuwa msongamano. Sie tofauti lakini tumezoea kwani tuko Europa Ligi!”