Sunday, December 4, 2016

LIGI KUU ENGLAND: LEO GOODISON PARK NI EVERTON vs MAN UNITED, BOURNEMOUTH vs LIVERPOOL

LEO zipo Mechi 2 za EPL, Ligi Kuu England, ambapo huko Fitness Stadium Bournemouth wataikaribisha Liverpool na huko Goodison Park ni Everton na Manchester United.
Liverpool hivi sasa wapo Nafasi ya 3 na ushindi kwao utawafanya waishushe Arsenal kutoka Nafasi ya Pili na kushikilia wao wakibaki Pointi 1 nyuma ya Vinara Chelsea.
Bournemouth wako Nafasi ya 12.
Nao Man United, ambao wako Nafasi ya 7, wako Ugenini huko Goodison Park kucheza na Everton iliyo Nafasi ya 8 Pointi 1 nyuma ya Man United.
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Luke Shaw, Eric Bailly na Chris Smalling huku Kepteni Wayne Rooney ikiwa Kifungoni Mechi 1 lakini Paul Pogba na Marouane Fellaini, waliokuwa Kifungoni Mechi 1, sasa wako huru kucheza Mechin hii.