Saturday, December 3, 2016

FULL TIME: EL CLASSICO: BARCELONA 1 vs 1 REAL MADRID

Luis Suarez dakika ya 53 kipindi cha pili anaipachikia bao Barcelona kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu frii kiki.
Zikiwa zimebaki dakika chache kumalizika Real walisawazisha kupitia kwa kichwa cha Sergio Ramos na kipute kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Real Madrid wameendelea kuongoza Ligi wakiwa kileleni.
Mtanange wa El Clasico uliochezwa huko Nou Camp Wenyeji Barcelona walikosa ushindi baada ya Real kusawazisha Dakika za mwishoni kabisa na Gemu kwisha 1-1.
Bao la Barca lilifungwa Dakika ya 53 na Luis Suarez kwa Kichwa alipounganisha Frikiki ya Neymar kutoka upande wa kushoto.
Baadae Barca walipata nafasi mbili za Bao za wazi na Neymar na Lionel Messi kupiga nje.
Huku Dakika zikiyoyoma Frikiki ya Luka Modric kutoka kushoto iliunganishwa kwa Kichwa na Sergio Ramos na kumshinda Ter Stegen na kutinga wavuni na kuiandikia Bao Real. Mara baada ya Bao hilo Frikiki ya Barca ilileta kizaazaa Golini mwa Real na Kipa Navas kuupanchi Mpira uliorudishwa kwa Kichwa Golini Sergi Roberto na Kiungo wa Real Casemiro, alieingizwa Kipindi cha Pili, kuokoa Mstarini.

Sare hii imewabakisha Real kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Barca ambao ni wa pili.