Saturday, December 17, 2016

FULL TIME EPL: CRYSTAL PALACE 0 v 1 CHELSEA, DIEGO COSTA AIPA USHINDI BLUES TENA LEO NA KUWA ZAIDI KILELENI

Chelsea Leo huko Selhurst Park wameifunga Crystal Palace 1-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 9 mbele.
Huo ni ushindi wa 11 mfululizo kwenye EPL wakiwania kuivunja Rekodi ya Arsenal ya kushinda Mechi 14 mfululizo iliyowekwa Mwaka 2002.
Bao la ushindi la Chelsea lilifungwa kwa Kichwa na Diego Costa katika Dakika ya 43 alipounganisha Krosi ya Cesar Azpilicueta.
Chelsea sasa wana Pointi 43 wakiwa wamecheza Mechi 1 zaidi ya Liverpool, walio Nafasi ya Pili, na Arsenal, walio Nafasi ya 3, zote zikiwa na Pointi 34 kila mmoja.
Jumapili Arsenal watacheza na Manchester City huko Etihad wakati Liverpool wakienda huko Goodison Park kucheza na Everton Jumatatu Usiku katika kimbembe cha Dabi ya Merseyside.