Monday, December 26, 2016

MANCHESTER UNITED 3 vs 1 SUNDERLAND, MKHITARYAN AREJEA NA KUFUNGA BAO LA KIWANGO, MOYES AKIKARIBISHWA OLD TRAFFORD!

Daley Blind dakika ya 39 kipindi cha kwanza ndiye aliyeanza kuzifunua nyavu za Sunderland.

Manchester United imepata ushindi wa nne mfululizo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo walioutawala dhidi ya Sunderland inayobakia katika mstari wa kushuka daraja baada ya kulala kwa magoli 3-1.
Manchester United iliyostahili ushindi iliutawala mchezo huo kwa asilimia 63, ilipiga mashuti 25 kwenye goli, lakini zilikuwa jitihada za beki Daley Blind zilizozaa matunda na kuipatia goli la kwanza kufuatia pasi ya Zlatan Ibrahimovic.
Katika kipindi cha pili Zlatan Ibrahimovic aliongeza goli la pili akinasa pasi ya Paul Pogba huku Henrikh Mkhitaryan aliyetokea benchi akifunga goli la kisigino licha ya kuonekana ameotea.


Zlatan Ibrahimovic akianza kushangilia goli wakati mpira ukielekea wavuni

Mchezaji raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan akifunga goli kwa kisigino United wameitandika Sunderland 3-1 katika Mechi ya kwanza kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.
Huo ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Man United katika EPL na Bao zao zilipachikwa na Daley Blind, Zlatan Ibrahimovic Na Bao tamu sana la alieanzia Benchi Henrikh Mkhitaryan.

Manchester United's Daley Blind (C) is congratulated by team mates after scoring their first goal with
VIKOSI

Man Utd:
De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Blind, Ander Herrera, Carrick, Pogba, Mata, Ibrahimovic, Lingard.
Akiba: Martial, Smalling, Rashford, Romero, Mkhitaryan, Fellaini, Darmian.

Sunderland: Pickford, Jones, Djilobodji, Kone, Van Aanholt, Larsson, Ndong, Denayer, Anichebe, Borini, Defoe.
Akiba: Mannone, Khazri, O'Shea, Love, Asoro, Honeyman, Embleton.

Refa: Martin Atkinson (W Yorkshire)
Manchester United's Zlatan Ibrahimovic in action with Sunderland's Papy DjilobodjiZlatan Ibrahimovic holds his ankle Zlatan Ibrahimovic holds his ankle
Juan Mata and Lamine Kone colide Billy Jones of Sunderland and Jesse Lingard of Manchester United compete for the ballSunderland manager David Moyes and Manchester United manager Jose Mourinho on the touchlineJose Mourinho greets David Moyes Manchester United mascot Fred the Red and Sunderland manager David Moyes