Sunday, December 4, 2016

FULL TIME..EVERTON 1 vs 1 MANCHESTER UNITED, HAKUNA MBABE!

WENYEJI Everton wamepata Sare ya 1-1 walipocheza na Manchester United huko Goodison Park kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, kwa msaaada wa Penati ya Dakika ya 89 iliyotolewa na Refa Michael Oliver.
Man United walitangulia kufunga katika Dakika ya 42 kwa Bao safi la Zlatan Ibrahimovic alipomvisha kanzu Kipa Stekelnburg alietoka Golini kuufuata Mpira ambao uligonga Posti ya juu, ya pembeni na kisha kuvuka mstari huku Beki wa Everton akiuokoa lakini Bao hilo kuthibitishwa na Mfumo wa Kielotriniki wa GLD, Goal Line Decision.

Kipindi cha Pili Man United wangeweza kupata Bao la Pili baada ya Shuti la Ander Herrera kupita Posti na kutoka.
Ndipo ikaja bahati ya Mtende ya Everton kwa Fowadi wao Gana ‘kujigonga’kwa Marouane Fellaini na Refa kuwapa Penati ambayo Leighton aliisawazishia Everton.