Saturday, December 17, 2016

FULL TIME: WEST BROM ALIBION 0 vs 2 MANCHESTER UNITED, ZLATAN IBRAHIMOVIC AIPA USHINDI UNITED UGENINI

Zlatan Ibrahimovic Leo amepiga Bao 2 huko The Hawthorns wakati Manchester United inaichapa West Bromwich Albion 2-0 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Bao hizo zimemfanya Ibrahimovic afikishe Bao 10 katika Mechi 9 na kuifanya Man United ifungane kwa Pointi na Timu ya 5 Tottenham ambao Jumapili wanacheza na Burnley.

Bao la Kwanza la Man United lilifungwa Dakika ya 5 kufuatia Krosi safi ya Jesse Lingard kuunganishwa kwa Kichwa na Ibrahimovic na kumhadaa Kipa Ben Forster ambae huko nyuma aliwahi kuwa Man United.
Dakika ya 56, Ibrahimovic alifunga Bao la Pili na kuipa Man United uongozi wa 2-0 uliodumu hadi mwishoni.
Ushindi huo umeifanya Man United iwe haijafungwa katika Mechi 10 za Mashindano yote.
WBA wanabaki Nafasi ya 7.

VIKOSI:
West Brom:
Foster; Dawson [Morrison, 74’], McAuley, Olsson, Nyom; Yacob, Fletcher; Brunt, Chadli [Leko, 82’], Phillips [Robson-Kanu, 81’]; Rondon
Akiba: Myhill, Robson-Kanu, Morrison, Gardner, McClean, Galloway, Leko
Manchester United: De Gea; Valencia, Jones, Rojo, Darmian; Carrick, Herrera [Smalling, 92’]; Lingard [Rashford, 77], Pogba, Rooney [Fellaini, 84’]; Ibrahimovic.
Akiba: Romero, Blind, Smalling, Fellaini, Mata, Martial, Rashford
REFA: ANTHONY TAYLOR
1-0