Monday, December 5, 2016

MAN CITY, CHELSEA KWA PILATO FA KWA VURUGU ZA WACHEZAJI WAO!

Manchester City na Chelsea zimefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji wao kufuatia vurugu za Wachezaji hao mwishoni mwa Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Jumamosi Uwanjani Etihad na Chelsea kushinda 3-1.
Rabsha hiyo ya Wachezaji wa Timu hizo ilitokea Dakika za Majeruhi, Dakika ya 95, wakati Fowadi wa City, Sergio Aguero, alipomchezea Rafu mbaya Beki wa Chelsea David Luis na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na tukio kusababisha Wachezaji kuvaana na Kiungo wa City Fernandinho kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada kuvamiana na Mchezaji wa Chelsea Cesc Fabregas ambae hatachukuliwa hatua yeyote.

Wote, Aguero na Fernandinho, watakuwa Kifungoni kwa Aguero kuwa ‘Jela’ Mechi 4 na Fernandinho Mechi 3.
Lakini kwa vile Aguero alishawahi kufungiwa Mechi 3 Mwezi Agosti kwa kumpiga kiwiko Mchezaji wa West Ham Winston Reid, Kifungo cha sasa kimeongezwa Mechi 1 zaidi.
Kifungo hicho cha Aguero kitamfanya azikose Mechi za City dhidi ya Leicester, Watf ord, Arsenal na Hull.
Man City na Chelsea zimepewa hadi Saa 3 Usiku Desemba 8 kujibu Mashitaka yao.