Saturday, December 31, 2016

MAPINDUZI CUP: YAANZA, TAIFA JANG’OMBE YAWATUNGUA ‘WAPINZANI WAO’ JANG’OMBE BOYS BAO 1-0 DAKIKA ZA MAJERUHI.

MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ya kuenzi Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba yameanza Usiku huu huko Amaan Stadium, Zanzibar kswa Timu pinzani kucheza na Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0 kati Mechi ya Kundi A.
Bao la ushindi la Taifa Jang’ombe lilifungwa Dakika ya 83.
Michuano yapo na Makundi Mawili na Kundi A lina timu za Simba ya Dar es Salaam, Taifa ya Jang’ombe, Jang’ombe Boys, KVZ na Mabingwa Watetezi, URA ya Uganda.
Kundi B lina Timu za Yanga, Azam FC, Jamhuri na Zimamoto.

MAKUNDI:
KUNDI A

-Simba
-Taif Jang'ombe
-Jang’ombe Boys
-KVZ
-URA [Mabingwa Watetezi, Toka Uganda]

KUNDI B
-Yanga
-Azam FC
-Jamhuri
-Zimamoto


Baada ya Mechi hii ya Leo, Januari 1 Mabingwa Watetezi, URA watacheza na KVZ kuanzia Saa 10 Jioni na baadae Simba kumenyana na Taifa ya Jang'ombe Saa 2 na Nusu Usiku.

Mechi za Kundi B zitaanza Januari 2, kwa Azam FC kucheza na Zimamoto kuanzia Saa 10 Jioni na Yanga kuivaa Jamhuri Saa 2 na Nusu Usiku.

KOMBE LA MAPINDUZI
Ratiba/Matokeo:
Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017
KVZ VS URA (Saa 10:00 jioni)
Simba vs Taifa Jang'ombe (Saa 2:30 usiku)
Januari 2, 2017
Azam vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni
Yanga vs Jamhuri (Saa 2:30 usiku)

Januari 3, 2017
Jang'ombe Boys vs URA (Saa 10:00 jioni)
KVZ vs Simba (Saa 2:30 usiku)

Januari 4, 2017
Zimamoto vs Yanga (Saa 10:00 jioni)
Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

Januari 5, 2017
KVZ vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)
Simba vs URA (Saa 2:30 usiku)

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe vs KVZ (Saa 2:30 usiku)

Januari 7, 2017
Jamhuri vs Zimamoto (Saa 10:00 jioni)
Yanga vs Azam (Saa 2:30 usiku) 


Januari 8, 2017
Simba vs Jang'ombe Boys (Saa 10:00 jioni)
Taifa Jang'ombe vs URA (Saa 2:30 usiku).

Januari 10, 2017
Nusu Fainali
Nusu Fainali ya kwanza (Saa 10: 00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili (Saa 2:30 usiku)
Januari 13, 2017
FAINALI

Saa 2: 30 usiku.